Saturday, August 17, 2013

FILAMU YA "FOOLISH AGE" YA LULU KUZINDULIWA 30 AGOSTI NDANI YA MLIMANI CITY


MSANII mwenye kipaji cha hali ya juu nchini na mwenye umri mdogo, Elizabeth Michael "LULU" anatarajia kuzindua filamu yake ya kwanza toka alipotoka gerezani, iitwayo "Foolish Age".

Filamu hii imetengenezwa na kampuni ya Proin Promotions Limited na itazinduliwa mnamo tarehe 30 Agosti 2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Filamu hiyo inayoelezea maisha ya Lulu ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na kutengenezwa na kampuni ya mahiri ya Proin Promotions Limited.

Katika uzinduzi huo, wasanii mbalimbali wakiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na bendi yake ya Machozi anatarajiwa kushusha bonge la burudani siku hiyo.

Kupitia mtandao wa kijamii, Lulu aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!! nina furaha ya kuwafahamisha kuwa tarehe  30/08/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE..... Hatimaye narudi kazini!!! Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY..... kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki..... na pia LADY JAYDEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!! nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....*PROINPROMOTERS"

Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya filamu nchini.  Filamu hii imetengenezwa na itasambazwa na kampuni ya Proin Promotions Limited.

Usikose uzinduzi huu utakaofanyika ndani ya ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 Agosti 2013.

Wednesday, March 6, 2013

TASWIRA YA MIKUMI LEO




Picha ya twiga kama alivyokutwa leo maeneo ya Mikumi.
(Picha zote na Shabani Tolle)

Wednesday, January 2, 2013

MSANII WA FILAMU, JUMA KILOWOKO (SAJUKI) AFARIKI DUNIA

Marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) baada ya kutoka India kwenye matibabu.

Marehemu Sajuki akiwa na Mkewe Wastara enzi za uhai wake.


Msanii wa filamu, Juma Kilowoko (a.k.a. Sajuki) amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Tabata Bima na anatarajiwa kuzikwa kesho kutwa Ijumaa tarehe 4 Januari 2013 katika makaburi ya Kisutu.

Sajuki alianza kuugua mwaka jana ambapo alipata matibabu kwenye Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam na kubainika ana uvimbe tumboni. Hata hivyo, afya yake ilizidi kwenda mrama na kusababisha kushindwa kutembea.

Wadau, mashabiki wake, ndugu, jamaa na marafiki walimchangia fedha ili apelekwe kutibiwa nchini India ambapo Mei 2012 alisafirishwa kwenda nchini humo na kufanyiwa upasuaji na kurejea baada ya wiki mbili akiwa na hali ya kuridhisha.

Tuesday, November 27, 2012

MSANII SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA

Marehemu Hussein Ramadhani Mkieti a.k.a. Sharo Milionea


Muigizaji, mchekeshaji na mwanamuziki Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a. Sharo Milionea amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Maguzoni Songa lililopo katika kijiji cha Lusanga wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Akithibitisha tukio hilo kupitia Clouds FM Radio kupitia kipindi cha Ala za roho kinachoendeshwa na mtangazaji Diva loveness love, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Constantine Massawe  amesema kuwa marehemu Sharo amepata ajali majira ya saa 2.00 usiku akiwa peke yake anaendesha gari aina ya Toyota Harrier na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Muheza.

“Leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera-Muheza mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzoni Songa wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake.  Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”


Naye mama mkubwa wa marehemu, bi. Fatma Mkieti akiongea na Redio Clouds FM amethibitisha kutokea kwa kifo hicho...

"Tulipopata hizo habari tulienda hospitali ya wilaya ya Muheza kwenda kuhakikisha.  Hatukufanikiwa kuuona mwili bali daktari ametuonesha picha zake ndipo tukathibitisha kuwa ni kweli ni yeye Sharo Milionea ndiye aliyefariki.  Msiba upo nyumbani Lusanga, Muheza na kwa vile marehemu alikuwa ni mtu wa watu, familia imepanga azikwe siku ya Jumatano ili kuwapa nafasi waliopo mbali kuweza kuhudhuria mazishi yake," amesema.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Hussein Mkieti (Sharo Milionea). Amen.

Thursday, October 11, 2012

JANETH JACKSON KUOLEWA 2013

Mwanamuziki Janeth Jackson (46) wa Marekani anatarajia kuolewa mwaka 2013 na tajiri wa kiarabu ajulikanaye kwa jina la Wissam Al Mana ambaye inasemekana kuwa alianza uhusiano nae wa kimapenzi mwaka 2010.

Mwanamuziku huyo anatarajiwa kubadilisha dini na kuwa muislam wakati wowote kabla ya ndoa yao.

Pichani, Janeth akiwa na vazi la baibui na mtandio, vazi ambalo ni maarufu sana kwa
wanawake wa kiislamu. 

 Janeth Jackson akiwa mitaani na vazi la kiislamu.

Wednesday, October 3, 2012

DIAMOND PLATINUMZ ASAINI MKATABA NA KAMPUNI YA I-VIEW STUDIOS YA DSM

KMSANII Naseeb Abdul almaarufu "Diamond Platinumz" ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya jijini Dar es Salaam ili wasimamie kazi zake zote za usanii kwa muda wa miaka miwili.

Kulingana na mkataba huo, kampuni ya I-View itakuwa ikisimamia maonesho, matangazo, nyimbo za kwenye simu (caller tunes & ringback tones), mavazi pamoja na mambo yote yahusuyo kazi zake za usanii, hivyo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo, mtu au kampuni yoyote itakayotaka kufanya kazi na msanii huyo itatakiwa kuwasiliana na kampuni hiyo.

“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo na kila kitu ambacho kinahusiana na yeye kinapaswa kupitia I-View,” amesema Peter Mwendapole, Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ambao ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo.

Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View na tayari usaili umeshafanyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video ya wimbo huo.

I-View ni kampuni inayoshughulika na kazi za kupiga picha, kutengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango na ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.

 Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu kama "Diamond Platinumz" akisaini mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya I-View Studios.  Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Raqey Mohammed. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View
 Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Peter Mwendapole.

 Diamond akipeana mkono na Raqey mara baada ya kusaini na kukabidhiana mkataba huo.

MASTAR WA BONGO BWANA, UTADHANI HAWANA WAZAZI??!!

What is this now?? Ikiwa kioo cha jamii anafanya hivi, jamii itegemewe kuwa vipi?

Haya! Nini hii sasa?? Si unajidhalilisha tu kisa kutaka umaarufu!!

RIHANNA NA VIATU VYA NGOZI YA ANACONDA

Mwanamuziki Rihanna akiwa anashuka kwenye gari huku akiwa amevalia viatu vilivyotengenezwa na ngozi ya nyoka aina ya Anaconda anayepatikana katika misitu ya Amazon iliyopo America Kusini.



Viatu hivi vinasemekana kugharimu takribani shilingi milioni 3 za kitanzania.

Friday, April 13, 2012

VITABU VYA HISTORIA YA KANUMBA VYAUZWA MITAANI

Ikiwa ni siku tatu zimepita tangu aliyekuwa msanii nguli wa filamu nchini, Marehemu Steven Charles Kanumba azikwe tarehe 10 Aprili 2012, vitabu vya historia yake vimeanza kuonekana mitaani vikiuzwa.

Vitabu hivyo vinavyouzwa kwa bei ya Sh. 3,000/= vimeonekana sehemu mbalimbali ikiwemo maeneo ya mataa ya Ubungo ambapo mwandishi wa habari hii aliviona.

Haijajulikana mara moja kama vitabu hivyo vimetengenezwa na kuuzwa kwa idhini kutoka kwa ndugu wa marehemu au la, kufuatia tangazo lililotolewa leo katika vyombo vya habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi ya msanii huyo, ndugu Mtitu kwamba mtu yoyote hana ruhusa ya kutengeneza au kuuza kitu chochote kinachohusiana na marehemu Kanumba bila ya idhini kutoka kwa familia ya marehemu huyo.

Marehemu Steven Charles Kanumba alifariki ghafla usiku wa tarehe 7 Aprili 2012 nyumbani kwake Sinza Vatican baada ya kuanguka chumbani kwake akiwa na msanii mwenzie Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Thursday, March 15, 2012

MWANAMKE AMNYANYASA MWANAE KIJINSIA, DAR

Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni!!

Mwanamke huyo pichani mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akimfanyia vitendo vya usagaji mwanae wa kike wa kumzaa mwenye umri wa miaka 7 kwa kumwingiza uume wa bandia katika sehemu zake za siri, mbele na nyuma na kumharibu vibaya katika sehemu hizo.

Kwa maelezo ya mama huyo, huyo ndio mtoto pekee aliye nae na alimpata kwa kubakwa na mwanaume akiwa anasoma kidato cha kwanza ambapo hadi leo baba wa mtoto hajafahamika.  Imegundulika pia kuwa mama huyo amekuwa akiwafanyia hivyo hata watoto wengine.

Inasemekana kuwa mwanzoni mama huyo alipoulizwa hakushtuka kusikia kuwa mwanae kaharibika na alikataa kuwa sio yeye aliyemfanyia kitendo hicho mwanae. 

Baada ya kupewa kichapo na wananchi ndipo alianza kulia na kukubali kuwa ni yeye ndie aliyemfanyia hivyo mwanae na hajielewi ni kwanini anafanya hivyo.

Pia katika kutapatata mama huyo aliomba apelekwe jela au awekwe mahali peke yake asionane na mtu yoyote au auawe kwa sababu hajitambui kwa nini anafanya hivyo.

Taarifa ya unyanyasaji jinsia wa mtoto huyu ilirushwa leo katika kipindi cha Leo Tena - Hekaheka cha redio ya Clouds kinachorushwa kuanzia saa 5.15 asubuhi.

Kwa taarifa zaidi pitia katika address ifuatayo:

Wednesday, February 15, 2012

Whitney Houston Family Told She Died from Rx NOT Drowning


Whitney Houston's family was told by L.A. County Coroner officials ... the singer did not die from drowning, but rather from what appears to be a combination of Xanax and other prescription drugs mixed with alcohol ... this according to family sources.

We're told Coroner's officials informed the family there was not enough water in Whitney's lungs to lead to the conclusion that she drowned.

Our sources say the family was told Whitney may well have died before her head became submerged.

And family sources tell us ... it was actually Whitney's aunt, Mary Jones, who discovered Whitney's body in the bathtub. Mary had laid out Whitney's dress for the evening on the bed and then left for about a half hour. When Whitney didn't come out of the bathroom, Mary entered, pulled Whitney out of the tub and began administering CPR.

And we're told ... Whitney's mom has arranged to have the singer's body flown back to Atlanta, as early as tomorrow. The family was told the Coroner has no problem releasing the body because there is no evidence of foul play --  and unless cops put a hold on the body, it can be flown back East.

For more details please visit: http://www.tmz.com/2012/02/13/whitney-houston-cause-of-death-prescription-drugs-drowning-atlanta/

Sunday, February 12, 2012

SINGER WHITNEY HOUSTON DIES AT 48



The superstar singer and actress's publicist, Kristin Foster, broke the news of Houston's passing to the AP, but thus far, no cause of death has been revealed.


Hotel sources have told the website that she was found by her bodyguard, and that despite attempts to resuscitate her, she was pronounced dead at 3:55pm local time on Saturday afternoon. She was due to perform at a pre-Grammy award party in Los Angeles last night.

Police in Los Angeles said that Houston and her entourage, which included friends, family and co-workers, had taken up a "fair portion" of the hotel's fourth floor.

"She was pronounced dead at the hotel and a number of people were able to identify her," Lieutenant Mark Rosen from Beverly Hills Police told the BBC.

"We still have detectives and crime scene investigators at the hotel, we are looking into the matter as a death investigation its not a crime scene at this time," he added.

At her peak in the 1980s and 1990s, Houston was the golden girl of the music industry and one of the world's best-selling artists.

Among her hits were How Will I Know, Saving All My Love for You and I Will Always Love You.
She won multiple Grammys including album and record of the year and her success carried her beyond music to movies like The Bodyguard.

But by the end of her career, drug use took its toll as her record sales plummeted and her voice became raspy and hoarse.

MAY HER SOUL REST IN PEACE, AMEN.

For more details please visit http://www.huffingtonpost.co.uk/2012/02/11/whitney-houston-dead-caus_n_1270915.html

Picha na habari na Huff Post Entertainment - UK