Wabunge nchini Senegal wameingia katika sakata la kurushiana
makonde na viti siku huku mmoja wao akimpiga kofi Mbunge wa kike usoni kutokana
na mjadala wenye ukinzani kushamiri wakati wa kikao cha majadiliano Bungeni.
Hata
hivyo, tukio hili linatokea wakati wa upigaji kura wa bajeti ya Wizara ya
sheria ya mwaka ujao (2023), ukifanyika na uwasilishwaji wa bajeti ukiendelea
huku Mbunge wa upinzani, Massata Samb alimpiga Amy Ndiaye Gniby wa muungano
tawala wa Benno Bokk Yakaar (BBY).
Gniby
alilipiza kwa kurusha kiti upande wa Samb kabla ya mbunge mwingine kumvuta hadi
sakafuni na kupelekea kikao hicho kusitishwa lakini hata hivyo wabunge hao
waliendelea kurushiana makonde na matusi.
Mzozo huo, ulitokea huku kukiwa na uhasama kati ya wanasiasa wa
chama tawala na cha upinzani huku Wanaharakati wa wanawake na wanachama wa
muungano unaotawala wakionesha kukerwa na shambulio la kimwili dhidi ya Ndiaye.
Wanaharakati
hao, wamesema wataendesha kampeni ya uhamasishaji kuhusu unyanyasaji dhidi ya
wanawake na wasichana kwakua tukio hilo limechukua taswira mpya na kusambaa
kote ulimwenguni kitu ambacho kinaweza kuleta athari na mkanganyiko.
Mvutano kati ya wanasiasa watawala na wa upinzani umekuwa ukiongezeka ambapo uchaguzi wa wabunge wa Julai, 2022 ulishuhudia chama tawala kikipoteza wingi wake wa kura kutokana na uwepo wa hofu kwamba Rais Macky Sall atawania muhula wa tatu mwaka wa 2024.
Source: Dar24 Blog
No comments:
Post a Comment