KMSANII Naseeb Abdul almaarufu "Diamond Platinumz" ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya jijini Dar es Salaam ili wasimamie kazi zake zote za usanii kwa muda wa miaka miwili.
Kulingana na mkataba huo, kampuni ya I-View itakuwa ikisimamia maonesho, matangazo, nyimbo za kwenye simu (caller tunes & ringback tones), mavazi pamoja na mambo yote yahusuyo kazi zake za usanii, hivyo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo, mtu au kampuni yoyote itakayotaka kufanya kazi na msanii huyo itatakiwa kuwasiliana na kampuni hiyo.

“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo na kila kitu ambacho kinahusiana na yeye kinapaswa kupitia I-View,” amesema Peter Mwendapole, Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ambao ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo.
Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View na tayari usaili umeshafanyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video ya wimbo huo.
I-View ni kampuni inayoshughulika na kazi za kupiga picha, kutengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango na ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.
Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu kama "Diamond Platinumz" akisaini mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya I-View Studios. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Raqey Mohammed. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View
Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Peter Mwendapole.
Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Peter Mwendapole.
Diamond akipeana mkono na Raqey mara baada ya kusaini na kukabidhiana mkataba huo.
No comments:
Post a Comment