Thursday, May 25, 2017

TANZIA: Mume wa Zari, Ivan Semwanga Afariki Dunia Leo


Aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’, Ivan Semwanga (39) amefariki dunia akiwa hospitali nchini Uganda alipokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo usiku wa kuamkia leo Mei 25, 2017.

Ivan, aliyekuwa baba wa watoto watatu wa kiume wa Zari, aliachana na mwanamama huyo miaka michache iliyopita ambapo Zari alihamishia mapenzi kwa mwanamuziki Diamond Platinumz ambaye mpaka sasa wamezaa  watoto wawili, wa kike mmoja na wa kiume mmoja.

Ivan alikuwa maarufu Afrika Mashariki kutokana na biashara zake kubwa alizokuwa akifanya zikiwemo umiliki wa vyuo mbali mbali nchini Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari ameandika yafuatayo:
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Ivan Semwanga. Amina.

No comments: