Thursday, April 6, 2017

NAPE KUWAELEZA UKWELI WOTE WAPIGA KURA WAKE WA MTAMA JUMAMOSI HII


ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnuye amesema kuwa Jumamosi hii jimboni kwake Mtama mkoani Lindi, ataeleza UKWELI WOTE wa yaliyomtokea siku za hivi karibuni.
Nape ambaye aliondolewa kwenye nafasi hiyo wiki chache zilizopita baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi ya Saa 24 aliyoiunda kufuatia Kituo cha Clouds TV kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Nape aliahidi kupeleka ripoti hiyo kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais John Pombe Magufuli ambapo siku iliyofuata Rais alimteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape.
Aidha Nape Nnauye alimshukuru Rais Magufuli kwa kumteua Mwakyembe kwenye nafasi hiyo na kuahidi kuendelea kuipa ushirikiano serikali.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nape ameandika;
“Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi tar 8/4/17” Nape

No comments: