Thursday, April 6, 2017

MSANII ROMA MKATOLIKI AVAMIWA STUDIO ZA TONGWE USIKU, AKAMATWA!

Taarifa iliyotolewa na Mbunge ambaye pia ni Rapa, Joseph Haule ‘ Prof. Jay’ kupitia ukurasa wake wa facebook imeeleza kuwa Rapa Ibrahim Mussa ‘ROMA Mkatoliki’ amevamiwa akiwa katika studio za Tongwe Records kisha kukamatwa na polisi ambao hawajafahamika mara moja.
“ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU…
Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONY @moni_ centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..
Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!  Ameandika Prof. Jay.

Juhudi za kumtafuta ROMA tangu alfajiri hazijafanikiwa mpaka sasa kwani simu yake inaita bila kupokelewa.
Wadau wa muziki wamekuwa wakiuliza wakitaka kufahamu ROMA amekamatwa kwa kosa gani na amepelekwa kituo gani cha polisi jambo ambalo jeshi la polisi halijaeleza mapaka sasa.
Chanzo: Global Publishers

No comments: