Thursday, April 6, 2017

JINSI YA KUITAFUTA NGOZI NZURI KWA KUTUMIA MATUNDA


LEO nitaongelea suala zima la binadamu kuwa na ngozi nzuri na yenye mvuto ambayo utaipata kwa kunywa maji ya matunda. Kama tulivyozoea, maji ya kunywa huwa yanatajwa kwenye kuing’arisha ngozi na kuondoa sumu mwilini mwa binadamu, sasa leo nitakufundisha jinsi ya kunywa maji mengi zaidi ambapo utatumia na matunda ili kuipata ngozi iliyo nyororo.
Chukua jagi lenye maji safi ya kunywa, changanya na limao, ndimu na vipande viwili vya tango, vyote vikiwa na maganda yake. Yaani usimenye. Hapa nikiongelea matunda simaanishi juisi yake bali namaanisha vipande ambavyo havijakatwa vya matunda hayo.
Hatua ya kwanza ni kuchanganya na maji hayo, hatua ya pili ni kuweka kwenye friji au pembeni yake kwa muda wa saa nane ili kupata ile ladha, kisha kunywa. Faida ya maji hayo
Kwanza; yatakusaidia kunywa maji kwa urahisi kwani yatakuwa na harufu nzuri na ladha inayonyweka zaidi ya maji matupu.
Pili;  yatasaidia kupunguza tumbo kwa wale wasiopenda matumbo makubwa au jina rahisi vitambi. Tatu;  yatasaidia kukupa ngozi nyororo yenye kuteleza. Kama utakosa matunda hayo, unaweza kutumia zabibu, tikiti maji, chungwa na strawberry.
Chanzo: Gazeti Amani

No comments: