Thursday, May 14, 2015

H-BABA AFUNGUKA KUHUSU KUMWEKA BLEACH KICHWANI MWANAE TANZANITE

Mtoto Tanzanite (kushoto) na mama yake, Flora Mvungi (kulia).
H.Baba na mwanae Tanzanite
H-baba akiwa na mwanae Tanzanite.
 Msanii wa bongo Fleva, H-Baba amewafungukia mashabiki wake waliomjia juu baada ya kumuweka dawa ya kubadilisha rangi nywele 'bleach' mtoto wake,Tanzanite mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mashabiki hao ambao kupitia mitandao mbalimbali ya jamii walimwambia msanii huyo kuwa bleach siyo nzuri kiafya kwa mtoto hivyo amekosea sana kufanya hivyo.

Akijibu lawama hizo, H-Baba amesema kuwa lazima mwanaye aishi kisanii kama wazazi wake na kwamba yeye kama mzazi hawezi kumuharibu mtoto wake.

'Watu wanashindwa kuelewa, Tanzanite ni mtoto wa wasanii baba na mama na pia sijampaka mwanangu bleach, hiyo ni hina.  Hina pia ni suna kwa dini yetu ya Kiislamu hivyo sioni tatizo hapo,'amesema H-Baba.
Chanzo: vitukovyamtaa.blogspot.com

No comments: