Thursday, May 14, 2015

LULU AKIRI NA KUTOA SABABU ZA KUPENDA KUTOKA NA WANAUME WANAOMZIDI UMRI

Lulu Akili na Kutoa Sababu ya Kupenda Kutoka na Wanaume Waliomzidi Umri
Msanii, Elizabeth Michael (Lulu).
Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amekiri kupenda kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume waliomzidi sana umri.

Akizungumza kwenye The Sporah Show, Lulu amezitaja sababu za kupendelea kutoka na wanaume waliomzidi umri.

SPORAH: Watu wanahisi kwamba Lulu anapenda sana kutembea na watu waliomzidi umri sana,

LULU: That’s true, sio uongo, sio sana, Napenda kudate mtu ambaye anayeweza kusimama kama mpenzi, kama kaka, kama baba, kama kiongozi. Sitakuwa tayari kuwa na ile relation leo tumeamka na Maisha Club, kesho tumeamka na Billicanas, kesho tumeamka pale tunakula chips, I need to gain from you, nje ya upenzi unanifundisha nini kwa sababu haimaanishi kwamba mi ntaishi na wewe milele, itafikia siku labda we utaondoka au mi ntaondoka, we ukiondoka mi nikibaki nimejifunza nini kutoka kwako na ntaendelea kuishi vipi.”

“Haimaanishi kwamba napenda kutembea na watu walionizidi umri labda miaka hamsini, napenda kuwa na mtu ambaye angalau ananizidi umri, ana uzoefu zaidi yangu, amepitia vitu vingi, anajua vitu vingi kwamba i’ll be there as a girlfriend lakini nakuwa naiba iba kidogo […] na vitu vingine vya kitoto kitoto vingi vinakuwa hamna.” amesema Lulu.

Chanzo: bongomovies.com

No comments: