Friday, September 13, 2013

BINTI AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA MGAHAWA ANAOFANYIA KAZI, DSM

Mwili wa marehemu Asha kama ulivyokutwa.
Majirani na watu mbalimbali waliofika katika eneo hilo kushuhudia.


Msichana mmoja aliyetambulika kwa jina la Asha Rashid Hussein amekutwa amekufa katika chumba ambacho huwa anafanya biashara ya vyakula katika eneo la mwananyamala Kisiwani karibu kabisa na bar ya Paradise.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne wakati binti huyo alipowasha moto katika chumba hicho Alfajiri kwa ajili ya kutengeneza chapati kwa ajili ya chai kwa wateja wake ambao kwa kawaida huwa wanakwenda kununua chai mahali hapo kila siku asubuhi.

Akisimulia jinsi alivyogundua tatizo hilo mama mwenye nyumba ambako tukio hilo limetokea,amesema alishangaa kuona hadi asubuhi ile mlango wa sehemu hiyo ya biashara ulikuwa haujafunguliwa na haikuwa kawaida kwa Asha kwani huwa anafungua mapema sana.

Alipojaribu kuusukuma akagundua kuwa mlango  huo ulikuwa umerudishwa tu na kuwekwa komeo dogo kwa ndani,walipochungulia ndipo akamuona bvinti huyo kalala huku chapati alokuwa anatengeneza ikiwa kwenye kibao na jikoni alikuwa kabandika chai.

Baadae polisi walipofika eneo la tukio walifungua mlango huo na kuuchukua mwili huo hadi katika hospitali ya Mwananyamala.

Diwani wa kata hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kupata ripoti ya daktari amesema sababu ya kifo cha binti huyo ni kuvuta hewa ya sumu inayotoka kwenye mkaa kabla haijakolea 'Carbon Monoxide' ambayo kwa kawaida kama ukiwasha mkaa na eneo husika likawa halina sehemu ya kutosha kupitisha hewa basi husababisha umauti kwa dakika chache sana.

Huu ndio mgahawa ambao marehemu Asha alikuwa akifanya kazi.
Mama mwenye nyumba akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo.
Mwili wa marehemu Asha ukiwa umewekwa katika gari tayari kwa kupelekwa Mwananyamala Hospitali.

Katika chumba alichokutwa Asha amekufa hakukuwa na dirisha hata moja na alijifungia wakati anawasha moto huo.

Binti huyo alizikwa juzi kijijini kwao huko kibaha mkoani pwani na habari zinasema alikuwa mgeni katika eneo hilo na ndiyo kwanza alikuwa ameletwa kwa ajili ya kufanya kazi ya mama lishe.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Asha Rashid Hussein mahali pema peponi, Amina.

No comments: