Monday, January 9, 2012

DARAJA LA KIGAMBONI KUJENGWA KARIBUNI

Na. Ipyana Mwaipaja
Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba wa kujenga daraja la Kigamboni na kampuni ya ujenzi ya China Jiangchang Engineering Co. (T) Ltd. ya China.

Mkataba huo umesainiwa jana na  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya ujenzi ya China, Shi Yuan katika hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Serena ya Dar es Salaam.

Akiongea katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo utagharimu shilingi bilioni 214 ambazo NSSF itachangia asilimia 60 na serikali ya Tanzania itatoa asilimia 40 iliyobakia.

"Asilimia 60 ya gharama za ujenzi wa daraja zitatolewa na NSSF na zipo tayari na asilimia 40 zitakazotolewa na serikali zipo tayari, sasa kama hela yote ipo kwanini ujenzi wa barabara ya kilomita nne uchukue miaka mitatu?" alisema Magufuli.


Waziri Magufuli akihutubia leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba
wa ujenzi wa daraja la Kigamboni. (Picha kwa hisani ya Michuzi blog)


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, akisaini mkataba wa ujenzi wa
daraja la Kigamboni katika hafla iliyofanyika jijini leo.  Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering Co. (T) Ltd.
ambayo ndiyo imeingia mkataba na NSSF, Shi Yuan. 
(Picha kwa hisani ya Michuzi blog) 

No comments: