Wednesday, January 15, 2020

MCHEZA NGOMA AFARIKI KWA KUNG'ATWA NA NYOKA

Image result for picha ya nyoka
James Paschal, Mkazi wa Mtaa wa Kilimani Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, ambaye ni mtaalamu wa sanaa ya kucheza na nyoka, amefariki dunia baada ya kung’atwa na nyoka, wakati akiwa porini akijaribu kuwakamata kwa ajili ya kazi yake.

Akizungumzia tukio hilo, mdogo wa marehemu Jefta Paschal ambaye aliambatana na marehemu porini kwa ajili ya mawindo, amesema kuwa walifanikiwa kumkamata nyoka huyo na wakiwa katika harakati za kumuweka kwenye mfuko maarufu kama sulphate, ndipo marehemu aling’atwa mkononi na nyoka huyo.

Baadhi ya majirani wa marehemu wamesema kuwa marehemu alifika nyumbani kwake akiwa katika hali mbaya na kuomba kupelekwa hospitali ambapo ghafla hali yake ilibadilika na kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimani, Frolence Mbabule amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa wananchi kuacha kuchezea wanyama wakali kama nyoka.

Chanzo EATV

No comments: