Tuesday, May 14, 2019

NANDY: RUGE ALIFARIKI MWEZI MMOJA KABLA YA NDOA YETU

Nandy, Ruge, alifariki ,mwezi ,mmoja ,kabla , ndoa ,FLY , THE ,WALL, Honouring ,Ruge, life ,death,
Ikiwa ni takribani miezi mitatu sasa tangu tasnia ya habari impoteze mmoja wa wadau wakubwa, Ruge Mutahaba, aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki amemkumbuka kwa namna yake akieleza jinsi kifo kilivyozima ndoto zao.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nandy ambaye jina lake halisi ni Faustina Charles, ameweka wazi kuhusu uhusiano wake na nguli huyo ambaye enzi za uhai wake alikuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group na kueleza kuwa walipanga kufunga ndoa Machi mwaka huu.

Jana akihojiwa na Millard Ayo, Nandy ameeleza uhusiano wao ulikuwa na siri kwa kuwa walikubaliana kulifanya suala hilo kuwa binafsi mpaka watakapokamilisha taratibu zote.

Amesema kuwa mara kadhaa alikuwa akikanusha uhusiano huo kwa kuwa waliona hakuna haja ya kuweka wazi.

"Hatukupenda uhusiano wetu uendeshwe na mitandao, tulikuwa tunajaribu kutengeneza njia ya maisha yetu binafsi ili kufikia lengo letu.  Hatukutaka life style (mtindo wa maisha) ya mahusiano ya awali ya Ruge yajitokeze kwenye maisha yetu."

Nandy ameeleza kuwa uhusiano wao ulianza baada ya yeye kuanza kumshirikisha Ruge katika vitu vingi na kwamba hata familia zao zote zilikuwa zikifahamu.

No comments: