Wednesday, October 17, 2018

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, January Henry Msofe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Mbali na Mwenyekiti huyo mpya wa Tume hiyo,  pia amewateua, Iddi Mandi na Julius Kalolo ambao wanakuwa Makamishna wa muda wa Tume hiyo.

Aidha, katika hatua nyingine, pia amemteua Paul Kimiti kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za Taifa (NARCO).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Uteuzi huo uliotangazwa jana Oktoba 16, 2018 na umeanza tangu Oktoba 14, 2018.

No comments: