Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe leo amewasilisha barua ya hoja binafsi kuunda Kamati ya Bunge ili ichunguze matukio mbalimbali yanayotishia umoja,usalama na mshikamano nchini. Nia hiyo ameieleza katika mtandao wa Tweeter ambayo iko hapa chini.
Hata hivyo, nia hiyo imeshutumiwa na watu kadhaa akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, aliyesema hatua hiyo ya Bashe ni ya “unafiki”, akimtaka mbunge huyo (Bashe) akikemee chama chake kirudishe uhuru wa kufanya mikutano kwa vyama vya upinzani, kuhakikisha watu hawatekwi na kuuawa.
Vilevile Mbunge wa Kigoma Mjini, akimjibu Bashe, alisema hatua hiyo ya mbunge huyo ni mwanzo mzuri na inabidi kuungwa mkono kwani ina nia njema.
Ujumbe wa Lema na Zitto pia tunauweka hapa chini:

No comments:
Post a Comment