Friday, February 16, 2018

MAJALIWA ATOA TAMKO HILI....


Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi yenye madarasa ya awali na kila tarafa iwe na shule ya kidato cha tano na cha sita.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na taaluma.

Waziri Mkuu Majaliwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo akiongozana na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  amezindua madarasa manne ya kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge wilayani  sengerema huko na kutoa maagizo hayo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameshtukia ubadhirifu katika mradi wa maji ambao unasimamiwa na halmashauri mbili za wilaya ya Sengerema na Buchosa ambapo ametoa maagizo kwa TAKUKURU wachunguze juu ya mradi huo.

No comments: