Friday, February 16, 2018

KAULI YA DKT SLAA BAADA YA KUAPISHWA



Balozi Mteule, Dkt. Wilbrod Slaa amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Shukrani hizo amezitoa leo Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa Balozi wa nchi hiyo ambapo amemuahidi kuwa hatomuangusha Rais Magufuli.

“Mh. Rais nafasi hii si rahisi sana kuiongoza lakini nitasema machache la kwanza ni la shukrani ni kwa Mungu aliyekuwezesha kuniona na kunipa majukumu haya ili niweze kukusaidia katika kazi hii ya Ubalozi lakini pia nikushukuru wewe Mh. Rais kwa imani uliyokuwa nayo kwangu bila shaka una vigezo vyako ulivyotazama naomba nisema sitakuangusha nitazingatia vipengele vyote vya kiapo na nitazingatia zaidi maslahi mapana ya taifa langu,” amesema Dkt. Slaa.

Ameongeza "Mh. Rais kwa kawaida mimi huwa sipendi kutoa ahadi lakini ahadi yangu kubwa ni kwamba nitatumia nguvu zangu zote kufanya yale yote ninayotakiwa kuyafanya kwa ajili ya taifa langu Mwenyezi Mungu akinisaidia na naomba tukishirikiana na timu ya wote tuliyonao kuanzia Mawaziri, Katibu Mkuu na wote tunaofanya kazi pamoja na mimi nawaahidi ushirikiano wangu, Mh. Rais baada ya kusema hayo sina mengi narudia tena asante sana Mh. Rais kwa kuniona , asante kwa kuniamini na kunipa majukumu haya naamini sitakuangusha nashukuru sana Mh. Rais."

No comments: