Friday, May 26, 2017

WOLPER ANG'AKA KUHUSIANA NA MADAI YA KUNUKA MWILI

Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’ ametokwa povu si la nchi hii baada ya kubanwa kuhusiana na madai ya kunuka mwili na kusema hajawahi kunuka maishani mwake na kwamba ingekuwa hivyo asingepapatikiwa na wanaume.

Wolper aliyaongea hayo hivi karibuni katika kipindi cha Shilawadu alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa runinga, Kwisa wa Kipindi cha SHILAWADU kinachorushwa na runinga ya Clouds.

Katika kuonesha kumaindi ile mbaya kuhusu madaia hayo, mrembo huyo ambaye kiukweli yuko bomba kwa muonekano alifunguka: “Aliyekuambia nanuka nani? Mimi sinuki wala sijawahi kunuka maishani mwangu, kuthibitisha hilo kwanza nisingekuwa napapatikiwa na wanaume kila kukicha sambamba na kuhongwa vitu kibao huku wengine nikiwaacha wakinililia.

Hao wanaosema na kusambaza hayo ni njia tu ya kujipatia followers kwenye mitandao yao kupitia mimi.” Wolper hakuishia hapo aliendelea kumwaga povu kuwa, tangu afungue duka la nguo ambalo amewekeza zaidi ya shilingi milioni 60, watu wengi wamekuwa wakichukizwa na maendeleo hayo. “Wana chuki tu na mimi, tangu nimefungua duka wananichokonoa, wanalishadadia hili jambo kisa tu nimepata mafanikio ya kufungua duka,” alipigilia msumari.
Chanzo: Ijumaa

No comments: