Tuesday, November 18, 2014

MAHOJIANO KATI YA MWANAMUZIKI YOUNG DEE NA WANA-MKASI SHOW

Mwanamuziki Young Dar es Salaam, a.k.a. Young Dee.
Kama hukuwa karibu na runinga yako jana wakati wa kipindi cha MKASI kinachorushwa na kituo cha EATV kuanzia saa 3.30 usiku hadi saa 4.00, haya ni mambo saba aliyoyazungumza mwanamuziki Young Dee kuhusiana na tatoo zake, anachofikiria kufanya kama akiacha muziki, msichana aliyemwimbia wimbo wa 'Siyo mchoyo', kukopi staili za muziki za wanamuziki wengine, kuhusu yeye na shule na kuhusu madawa ya kulevya.

Mmojawapo wa hosts wa kipindi cha Mkasi Show, Salama Jabir.
SALAMA: "Mara yako ya kwanza kuchora tatoo ulikuwa una miaka mingapi?"

YOUNG DEE: "Actually sikumbuki nilikuwa na miaka mingapi, tatoo yangu ya kwanza imeandikwa 'The City of David'... hii ndiyo project ambayo naifanya hadi sasa hivi kuanzia kwenye 'Dada anaolewa', 'Tunapeta' hadi sasa hivi nyimbo zangu zinazotoka ni project ambayo nimeanza kuifanya muda mrefu. Nina kama miaka mitano kama sikosei kwa hiyo miaka mitano iliyopita ndiyo nilichora tatoo yangu ya kwanza"

SALAMA:  "Wewe kwa jinsi ulivyo, unadhani utafanya muziki maisha yako yote? cha pili, kama ukiamua kuacha muziki na kufanya kitu kingine, pengine kufanya kazi benki, UN ama wherever, hauhisi kwamba maamuzi yako ambayo unayafanya sasa hivi yanaweza yakakugharimu kwa vitu vya baadaye?"

YOUNG DEE: "Sijawahi kufikiria kufanya kazi UN au benki wala nini, wala kuwa mwanajeshi.  Sijawahi kufikiria hivyo, wala sitamani, wala sita-enjoy na sitapenda na siwezi kufanya kitu ambacho sikipendi, lazima nifanye kitu ambacho nakipenda.  Hata kama hakinilipi kabisa kama nakipenda, naenjoy kukifanya then I will do it mpaka nitakapofariki"

MUBA: "Ule wimbo ulioutoa juzi unaoitwa 'Siyo Mchoyo' nimesikia baadhi ya watu wanaongea kwamba kweli kuna demu ambaye kabisa yupo, ni ukweli kwamba ulimwandikia demu yeyote?"

YOUNG DEE: "Huyo demu ndiyo yupo na siyo mchoyo kweli.  Mimi hata sikuutunga sana yaani kwa sababu nimechoka kutunga siku hizi, naongea kitu ambacho nakiona"

MUBA:  "Wanasemaga Young Dee anakopi sana staili, yaani unasikiliza nyimbo za akina Lil Wayne halafu unakuja kuchukua staili katika mashairi ya mtu. Ukweli ukoje kuhusu hili?"

YOUNG DEE:  "Sijawahi kukopi mashairi ya mtu.  Kusikiliza ni kweli nasikiliza sababu mimi muziki kwangu ni maisha yangu so lazima nisikilize muziki, mtu hawezi kunichagulia nini cha kusikiliza."

SALAMA: "Wewe ni kijana na umeanza kufanya kazi muda mrefu sana, niambie shule yako ikoje?"

YOUNG DEE: "Nimeishia O level, mambo ya kifamilia nikashindwa kuendelea tena so ikabidi nitafute ugali kwa staili nyingine, ndiyo ikawa hivyo.  Bado nafikiria kurudi shule lakini nitakapojua nini nakitaka shuleni, nikishaweka akili yangu hivyo then nitarudi shule."

SALAMA:  "Ni kitu gani ambacho kimeshawahi kukuumiza sana katika maisha yako?"

YOUNG DEE:  "Ni ishu kuhusu mimi kujihusisha na madawa ya kulevya. Mwanzo nilikuwa nikisikia inasemwasemwa ila nilichukulia kawaida sababu ni kitu ambacho si cha kweli ila nilipoona hadi washikaji zangu na watu wa karibu nao wanaonesha kunishuku kuhusu hilo ndo nikaona ni ishu ipo serious."

Mwanamuziki Young Dee (kushoto) akiwa na Crew nzima ya Mkasi Show.

No comments: