Friday, September 13, 2013

BINTI AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA MGAHAWA ANAOFANYIA KAZI, DSM

Mwili wa marehemu Asha kama ulivyokutwa.
Majirani na watu mbalimbali waliofika katika eneo hilo kushuhudia.


Msichana mmoja aliyetambulika kwa jina la Asha Rashid Hussein amekutwa amekufa katika chumba ambacho huwa anafanya biashara ya vyakula katika eneo la mwananyamala Kisiwani karibu kabisa na bar ya Paradise.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne wakati binti huyo alipowasha moto katika chumba hicho Alfajiri kwa ajili ya kutengeneza chapati kwa ajili ya chai kwa wateja wake ambao kwa kawaida huwa wanakwenda kununua chai mahali hapo kila siku asubuhi.

Akisimulia jinsi alivyogundua tatizo hilo mama mwenye nyumba ambako tukio hilo limetokea,amesema alishangaa kuona hadi asubuhi ile mlango wa sehemu hiyo ya biashara ulikuwa haujafunguliwa na haikuwa kawaida kwa Asha kwani huwa anafungua mapema sana.

Alipojaribu kuusukuma akagundua kuwa mlango  huo ulikuwa umerudishwa tu na kuwekwa komeo dogo kwa ndani,walipochungulia ndipo akamuona bvinti huyo kalala huku chapati alokuwa anatengeneza ikiwa kwenye kibao na jikoni alikuwa kabandika chai.

Baadae polisi walipofika eneo la tukio walifungua mlango huo na kuuchukua mwili huo hadi katika hospitali ya Mwananyamala.

Diwani wa kata hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kupata ripoti ya daktari amesema sababu ya kifo cha binti huyo ni kuvuta hewa ya sumu inayotoka kwenye mkaa kabla haijakolea 'Carbon Monoxide' ambayo kwa kawaida kama ukiwasha mkaa na eneo husika likawa halina sehemu ya kutosha kupitisha hewa basi husababisha umauti kwa dakika chache sana.

Huu ndio mgahawa ambao marehemu Asha alikuwa akifanya kazi.
Mama mwenye nyumba akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo.
Mwili wa marehemu Asha ukiwa umewekwa katika gari tayari kwa kupelekwa Mwananyamala Hospitali.

Katika chumba alichokutwa Asha amekufa hakukuwa na dirisha hata moja na alijifungia wakati anawasha moto huo.

Binti huyo alizikwa juzi kijijini kwao huko kibaha mkoani pwani na habari zinasema alikuwa mgeni katika eneo hilo na ndiyo kwanza alikuwa ameletwa kwa ajili ya kufanya kazi ya mama lishe.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Asha Rashid Hussein mahali pema peponi, Amina.

SHOGA (AUNT ASU) AOKOKA NA KUACHANA NA MAMBO YA KISHOGA

Aunt Asu enzi akiwa shoga.




Aliyekuwa shoga maarufu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Anti Asu (sasa anaitwa Amos) ameokoka rasmi na kuachana kabisa na shughuli hiyo ambayo ni kinyume kabisa na maadili yetu ya kitanzania.

Aunt Asu alitangaza uamuzi wa kuachana na ushoga na kumrudia Mungu katika kipindi cha Mitikisiko ya  Pwani cha kituo cha Times FM ambapo huwa ni mahususi kwa kupiga nyimbo za taarabu na habari zinazuhusu wanamuziki wa taarab na wadau wa muziki huo hapa nchini na kinaendeshwa na mtangazaji huyo Dida Shaibu mwenye masham sham mengi katika kukichagiza.

Watu kadhaa wameonekana kutoa maoni yao tofauti wakimpongeza kwa hatua yake hiyo huku wengi wakisema ama kwa hakika Mungu mkubwa na inapaswa woote wenye  tabia kama alizoziacha Aunt Asu waache mara moja na kumrudia Mungu.

Katika picha zake zilizooneshwa katika mitandao mbalimbali, watu wengi walionekana kutotambua kama aunt Asu ni mwanamke au mwanaume kutokana na mavazi ya kike aliokuwa ameyavaa lakini picha nyingine zinazomuonesha akiwa amevalia suti yupo kanisani mara baada ya kutangaza kuokoka ndizo zimefanya watu waamini kuwa ni mwanaume.

Picha za chini zinamuonesha Aunt Asu baada ya kuokoka na kuachana na mambo ya kishoga.



Aunt Asu (mwenye suti) baada ya kuokoka na kutangaza kuachana na mambo ya kishoga.

Sunday, September 8, 2013

DIAMOND AINGIA KATIKA SKENDO MPYA YA KUZALISHA NA KUTELEKEZA

MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano.

Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo.

Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo.

Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.

Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.

Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa.

Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo.

Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu.

Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.

Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.

‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.

Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia.

Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana.

Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya  na walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa.

Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao.

Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina.

Baada ya kupata madai hayo alitafutwa Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena,  naye aliacha kumfuatilia.

“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.

Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya kiganjani akiwa Nairobi, Kenya na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya ishu hiyo, alieleza:

“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”

Katika kuonesha ‘usiriazi’, mwandishi aliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha.

SOURCE: peruzibongo blog