Thursday, March 15, 2018

MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA MBELE YA IKULU


Wanafunzi nchini Marekani wameandamana kupinga hatua ya Bunge la Marekani kushindwa kufanya maamuzi ya kuzuia uvunjifu wa amani unaotokana na mashambulizi ya kutumia silaha katika shule za Marekani na kuwakumbuka wale waliouawa kwa bunduki mwezi Februari katika shule ya sekondari ya Florida.

Waandaaji wa maandamano hayo wamesema kuwa takriban wanafunzi 3,000 walipanga kutoka madarasani nchi nzima, wakati maandamano mengine yakifanyika mbele ya Ikulu ya White House na Bunge la Marekani.

Aidha, baadhi ya viongozi wa shule nchini Marekani wameunga mkono maandamano hayo, lakini wengine wamesema wanafunzi hao watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa masomo kwa kutoka nje ya madarasa bila ya kupewa ruhusa.

“Sisi hatuko salama tukiwa mashuleni. hatuko salama katika miji na vitongoji vyetu. Bunge lazima lichukue hatua za kuridhisha ili kutuhakikishia usalama wetu na lipitishe mabadiliko ya sheria za silaha katika serikali kuu,”wamesema waandamanaji hao.

Hata hivyo, wanafunzi hao wameandamana kupinga kitendo cha Bunge la Marekani kutochukua hatua yoyote zaidi ya kutuma ujumbe wa tweet na maombi kufuatia shambulizi la uvunjifu wa amani kwa kutumia bunduki lililoziathiri shule na wale wanaoishi katika maeneo jirani na shule hizo.

No comments: