Friday, November 24, 2017

MAMA KANUMBA KUMTAMBELEA LULU GEREZANI

Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
MAMA wa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kuwa, kutokana na matatizo yaliyompata staa wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili, amekuwa akimuonea huruma na anajipanga kumtembelea gerezani.

Mtegoa amesema watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa ana chuki na Lulu, lakini moyo wake unampenda na kama isingekuwa sheria kuhitaji Lulu kufungwa basi yeye asingekuwa na tatizo naye.
Staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu'.
“Sina chuki na Lulu, tulikuwa karibu lakini nafikiri watu wake wanaomzunguka ndiyo waliosababisha ukaribu wetu kuparaganyika," amesema mama Kanumba na kuongeza kuwa yeye ni Mkristo kwa hiyo hawezi kufurahia kuona mwenzie anapata matatizo hivyo atapanga siku na kwenda kumtembelea gerezani.

No comments: