Friday, September 22, 2017

WAETHIOPIA NANE WAKAMATWA MBAGALA


Idara ya uhamiaji nchini inawashikilia raia nane wa Ethiopia waliokuwa wanasafirishwa kwenda Mtwara kwa kutumia usafiri wa lori lenya namba za usajili T 181 DKB likiwa na trailer lenye namba za usajili T 961 DKA mali ya kampuni ya DANGOTE.

Kamishna wa utawala na fedha wa idara ya uhamiaji nchini amesema watu hao wamekamatwa eneo la Kongowe Mbagala wakiwa katika harakati za kusafirishwa kuelekea Mtwara ambapo idara hiyo pia inawashikilia watanzania wanne ambao wanadaiwa kushiriki kwenye mtandao huo wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Kamishna huyo wa uhamiaji ametoa wito kwa wamiliki pamoja na madereva wa malori na vyombo vingine vya usafiri kuacha kujihusisha na usafirishaji haramu wa binadamu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

No comments: