Thursday, May 14, 2015

MASHABIKI WACHUKIZWA NA PICHA ZA WAZI ZA AUNT EZEKIEL

Mashabiki Wachukizwa na Picha Hizi za Aunt Ezekiel
Hizi ndio picha za Aunt Ezekiel zilizowachukiwa mashabiki wake (juu na chini).
 
Staa wa bongo movies, Aunt Ezekiel amepondwa na baadhi ya mashabiki wake kwa kupiga picha hizi akionyesha tumbo lake ukizingatia yeye ni mjamzito.

Picha hizi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na wengi wameonesha kuchukizwa na tabia iliyozuka ya mastaa wa Bongo kufanya hivi kwa kuwaiga mastaa wa nchi za ughaibuni.

Wakati huo huo leo kupitia kipindi cha Amplifaya kinachorushwa na redio ya Clouds chini ya mtangazaji Millard Ayo, Mosse Iyobo ambaye ni mcheza shoo wa mwanamuziki maarufu nchini, Diamond, ameweka hadharani kuwa yeye ndiye mwenye ujauzito wa muigizaji huyo na kwamba ameshamtambulisha kwao.

Aunty 1
Mosse Iyobo

No comments: