Wednesday, January 2, 2013

MSANII WA FILAMU, JUMA KILOWOKO (SAJUKI) AFARIKI DUNIA

Marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) baada ya kutoka India kwenye matibabu.

Marehemu Sajuki akiwa na Mkewe Wastara enzi za uhai wake.


Msanii wa filamu, Juma Kilowoko (a.k.a. Sajuki) amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Tabata Bima na anatarajiwa kuzikwa kesho kutwa Ijumaa tarehe 4 Januari 2013 katika makaburi ya Kisutu.

Sajuki alianza kuugua mwaka jana ambapo alipata matibabu kwenye Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam na kubainika ana uvimbe tumboni. Hata hivyo, afya yake ilizidi kwenda mrama na kusababisha kushindwa kutembea.

Wadau, mashabiki wake, ndugu, jamaa na marafiki walimchangia fedha ili apelekwe kutibiwa nchini India ambapo Mei 2012 alisafirishwa kwenda nchini humo na kufanyiwa upasuaji na kurejea baada ya wiki mbili akiwa na hali ya kuridhisha.