Thursday, December 1, 2022

MWIMBAJI WA MAREKANI JAKE FLINT AFARIKI SAA CHACHE BAADA YA HARUSI

 

Marehemu Jake Flint enzi za uhai wake.


Hali ya sintofahamu inaendelea kutanda kuhusu kifo cha mwanamuziki wa taarabu nchini Marekani, Jake Flint, saa chache baada ya harusi yake siku ya Jumapili.

Flint, 37, alifariki usingizini huko Oklahoma, meneja wa zamani Brenda Cline alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii.

Heshima zimeanza kumiminika kwa mwimbaji huyo ambaye alichukuliwa kuwa nyota anayechipukia katika muziki aina ya “Red Dirt”, aina ya muziki wa taarabu kutoka Oklahoma.

Mke mpya wa Flint, Brenda Wilson Flint, amechapisha video ya wawili hao wakicheza chini ya mti siku ya harusi yao.

“Tunapaswa kupitia picha za harusi lakini badala yake lazima nichague nguo za kumzika mume wangu,” aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Facebook.

Wenzi hao walifunga ndoa katika sherehe huko Tulsa siku iliyotangulia.

“Kwa moyo uliovunjika na huzuni kubwa lazima nitangaze kwamba Jake Flint ameaga dunia,” meneja wa zamani Brenda Cline aliandika.

“Nimejaribu mara kadhaa leo kuweka ujumbe, lakini huwezi kutoa maoni juu ya kile ambacho huwezi kushughulikia.”

Mtangazaji wa muda mrefu Clif Doyal alithibitisha kifo hicho kwa gazeti la Oklahoman, akisema kwamba Flint alifariki usingizini.

“Sidhani kama nimewahi kukumbana na hali ya kushtua kama hii ya kupoteza mtu na jinsi hii ni ukatili kwa Brenda, mke

“Kuwa bibi na mjane katika masaa machache tu haiwezekani.”

Red Dirt, aina ya muziki wa taarabu, imepewa jina la rangi tofauti ya udongo katika jimbo la Oklahoma, ambapo Flint alizaliwa katika mji wa Holdenville kabla ya kuhamia Tulsa.

Source: Global Publishers

No comments: