Wizara
ya Sheria ya Marekani juzi ilimtaja mpelelezi wa zamani wa uhalifu wa kivita
kama Wakili maalum wa kusimamia uchunguzi wa uhalifu dhidi ya Donald Trump,
siku tatu baada ya Rais huyo wa zamani kutangaza kuwa atagombea tena uchaguzi
wa Rais wa mwaka 2024.
Trump,
ambaye anadai kuwa ‘anawindwa na wachawi’, alikashifu hatua hiyo akisema isiyo
ya haki na siasa chafu katika nchi yao huku Ikulu ilikanusha uingiliaji wa
kisiasa, lakini uchunguzi wa mawakili maalum wa Rais wa zamani na mgombea wa
sasa unaweka mazingira ya vita vya kisheria.
Katika
mkutano na waandishi wa habari, Mwanasheria Mkuu Merrick Garland alitangaza
uteuzi wa Jack Smith, ambaye alikuwa mwendesha mashtaka mkuu huko The Hague,
akichunguza uhalifu wa kivita wa Kosovo, kuchukua jukumu la chunguzi mbili
zinazoendeshwa dhidi ya Trump.
Uchunguzi
mmoja unaangazia juhudi za Rais huyo wa zamani za kutengua matokeo ya uchaguzi
wa 2020 na shambulio la Januari 6, 2021 dhidi ya Ikulu ya Marekani lililofanywa
na wafuasi wake.
Nyingine
ni uchunguzi wa hifadhi ya nyaraka za siri za Serikali zilizonaswa wakati
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) lilipovamia kwenye makazi ya Trump ya
Mar-a-Lago huko Florida Agosti mwaka huu.
Mwanasheria Garland alisema kumtaja wakili maalum ni kwa manufaa ya umma kwa sababu Trump wa chama cha Republican na mrithi wake wa Chama cha Democratic, Joe Biden wameeleza nia yao ya kugombea 2024, ingawa ni Trump pekee ndiye ametangaza rasmi kwa sasa.
No comments:
Post a Comment