Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi |
Baraza la
Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Desemba 1, 2022 limetangaza matokeo ya darasa
la saba kwa mwaka 2022 ambapo limetangaza kufuta matokeo yote ya Watahiniwa
2194 sawa na asilimia 0.16 ya Watahiniwa 1,350,881 waliofanya mtihani ambao
wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi
mwaka 2022.
Kati ya hao wasichana ni 558,825
ambao ni sawa na asilimia 78.91 na wavulana ni 514,577 sawa na asilikia 80.41.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi ametangaza matokeo hayo leo Alhamisi
Desemba Mosi, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa kuhusu mtihani
huo wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.
Almasi
amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na
asilimia 81.97.
Amesema
kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa
waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24
ikilinganishwa na mwaka jana.
Ili kupata matokeo hayo ingia kwenye link hii: https://matokeo.necta.go.tz/psle2022/psle.htm
Source: Global Publishers
No comments:
Post a Comment