Wednesday, January 29, 2020

PETIT MAN: SI VEMA KUANIKA MITANDAONI MAMBO YA FARAGHA

MENEJA wa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ahmed Manungwa ‘Petit Man’ amesema kwamba haoni kama kuna umuhimu wa kuyaanika matatizo yake yanayomkuta kwenye mahusiano. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Petit amesema kuanika matatizo ya mpenzi wake kwenye mitandao sio jambo jema ndiyo maana yeye huwa akikosana na mwenzi wake basi huyamaliza kimyakimya.

“Sioni kama ni jambo zuri kuzungumzia mambo yenu ya faragha mitandaoni, haijalishi mmekwazana kiasi gani, kwa sababu madhara yakuanika siri zenu hadaharani ni makubwa kuliko kukaa chini na kuyamaliza kimya kimya. Mpaka leo sijawahi kuzungumza sababu ya mimi kuachana na mwanamke ambaye nilimuoa na hata niliporudi kwa mzazi mwenzangu Esma Khan bado ilikuwa kimya kimya,” alisema Petit.
Chanzo: Global Publishers Online

No comments: