Padri wa Kanisa Katoliki, Dkt.
Bernard Msike ambaye aliwafungisha ndoa staa wa Hip Hop, Bonaventure
Kabogo ‘Stamina’ na mkewe Veronica Peter katika Kanisa la Mt. Maria
Consolata mkoani Morogoro, amewaita wanandoa hao kanisani kwa ajili ya
usuluhishi.
Padri huyo aliwafungisha ndoa hiyo Mei, 2018
ambayo imedumu kwa takriban mwaka mmoja na miezi kadhaa kisha kumwagana
na kuzua gumzo kama lote mitandaoni wiki iliyopita.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko baada ya sakata hilo kutikisa mitandaoni, Padri Msike alianza kwa kusema anasikitika kuona ndoa hiyo imedumu kwa muda mfupi kwani si kawaida yake kufungisha ndoa na kisha kuvunjika.
“Hii nafikiri itakuwa ndoa yangu ya kwanza au ya pili kuvunjika katika ndoa nilizofungisha,
imenishtua kwa sababu sikutegemea kama wanaweza kuachana ndani ya muda
mfupi namna hii,” alisema Padri Msike.
Padri huyo alisema atawaita wawili hao kanisani kwa ajili ya
usuluhishi kwani kanisa bado linaitambua ndoa yao.
“Niwaase tu katika
kipindi hiki wasije wakaanzisha mahusiano mapya maana watakuwa wanatenda
dhambi. Kanisa Katoliki linaitambua ndoa ya mwanaume na mwanamke mmoja
tu mpaka kifo kitakapowatenganisha,” alisema.
Stamina na mkewe wameachana na mkali huyo kutoa wimbo wa Asiwaze
ambao unatajwa kuwa amemsema mkewe huyo. Sababu kubwa inayotajwa katika
kuachana kwa wawili hao ni usaliti.
No comments:
Post a Comment