James Paschal, Mkazi wa Mtaa wa Kilimani Kata ya Nsemulwa Manispaa ya
Mpanda mkoani Katavi, ambaye ni mtaalamu wa sanaa ya kucheza na nyoka,
amefariki dunia baada ya kung’atwa na nyoka, wakati akiwa porini
akijaribu kuwakamata kwa ajili ya kazi yake.
Akizungumzia tukio hilo, mdogo wa marehemu Jefta Paschal ambaye aliambatana na marehemu porini kwa ajili ya mawindo, amesema kuwa
walifanikiwa kumkamata nyoka huyo na wakiwa katika harakati za kumuweka
kwenye mfuko maarufu kama sulphate, ndipo marehemu aling’atwa mkononi na nyoka huyo.
Baadhi ya majirani wa marehemu wamesema kuwa marehemu alifika
nyumbani kwake akiwa katika hali mbaya na kuomba kupelekwa hospitali ambapo ghafla hali yake ilibadilika na kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimani, Frolence Mbabule amekiri kutokea kwa
tukio hilo na kuwaasa wananchi kuacha kuchezea wanyama wakali kama
nyoka.
Chanzo EATV
No comments:
Post a Comment