MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans
Poppe, leo amefikishwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kujibu kesi inayomkabili ya madai ya kutoa taarifa za uongo
kuhusiana na malipo ya kodi, kifungu 106(1) A& C (i) cha Income Tax
Act sura ya 332 R.F 2008, kati ya Machi 10, 2016 na Septemba 30, 2016.
Poppe na mfanyabiashara, Franklin Lauwom wamefikishwa katika
mahakama hiyo, saa tatu na nusu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba
cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani.
Aprili 30, 2018, mahakama hiyo iliamuru washtakiwa Hans Poppe na Lauwo wakamatwe popote walipo.
Mahakama hiyo ilitoa amri hiyo baada ya upande wa mashtaka kupitia
kwa Wakili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard
Swai, kuieleza kuwa wamewatafuta washtakiwa hao tangu Machi 16 mwaka
huu bila mafanikio
Poppe alikamatwa juzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaamwakati akirejea nchini ambapo ameunganishwa kwenye kesi
inayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva, na Makamu wake Geofrey Nyange
‘Kaburu’.
No comments:
Post a Comment