Mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Chinindu Innocent, mkaazi wa
jimbo la Abia nchini Nigeria anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la
kumteka mama wa aliyekuwa mpenzi wake.
Innocent anashikiliwa pamoja na wenzake watatu waliohusika kwenye
tukio la utekaji huo, siku chache baada ya kupewa kiasi cha N300,000
kisha kumuachia mateka wao.
Kwa mujibu wa maelezo ya mahojiano kati ya Innocent na jeshi la
polisi, yaliyochapishwa na PUNCH, Innocent alieleza kuwa alichukizwa na
kitendo cha usaliti ambacho alifanyiwa na mpenzi wake na kisha akaamua
kwenda kumueleza mama yake [mama wa binti] ambaye walikuwa wanafahamiana
kwani alikuwa akitembelea nyumba hiyo.
“Kwanza nilipogundua nilizungumza na mtoto wake lakini mtoto wake
alitishia kuua uhusiano wetu. Kwakuwa nampenda sana nikaenda kumueleza
mama yake, lakini naye hakufanya kitu chochote, nikakasirika nikaamua
kupanga namna ya kuwaadhibu,” Innocent anakaririwa.
Alisema kuwa alizungumza na binamu yake aliyemtaja kwa jina la
Aparazu Ogwu ambaye walifikia muafaka kuwa wamteke mama wa mpenzi wake,
pamoja na mambo mengine wakilenga kupata fedha nyingi kama sharti la
kumuachia. Baada ya kukubaliana waliwatafuta watu wengine watatu ambao
ni genge la wahalifu ili wawasaidie.
No comments:
Post a Comment