Tuesday, October 16, 2018

HAJI MANARA AACHIWA KWA DHAMANA



MSEMAJI  wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa takribani siku nne.

Manara alishikiliwa kwa mahojiano siku moja tu baada ya kutekwa kwa mwanachama mwekezaji maarufu wa Simba, Mohamed Dewji.

Dewji maarufu kama Mo, alitekwa na watu wasiojulikana wakielezwa ni raia wa kigeni akiwa anaingia gym ya mazoezi kwenye Hoteli ya Collosseum eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam, alfajiri ya Alhamisi iliyopita.

No comments: