Canada imekuwa nchi ya pili baada ya Uruguay kuruhusu kisheria
matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi kwa ajili ya tiba
(recreational marijuana).
Soko la nchi hiyo linalouza bangi linafunguliwa rasmi leo usiku
wa ‘manani’, hali inayozua wasiwasi kuhusu madhara ya matumizi hayo
kiafya na kiusalama wa umma kwa ujumla. Tayari watu wameanza kununua
kwenye maduka ya rejareja wakipewa risiti zilizokatwa kodi.
Picha ya wanaodaiwa kuwa wa kwanza kununua marijuana katika eneo la St. John’s Newfoundland. |
Taarifa za sheria hiyo mpya imetumwa kwa wakazi zaidi ya milioni 15
kwa ajili ya kuwajulisha wananchi pamoja na kufanya kampeni ya udhibiti
wa matumizi yake kwa tiba.
Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kupitisha sheria ya kuruhusu matumizi
ya dawa hizo za kulevya kwa ajili ya tiba, ingawa Ureno na Netherland
walikuwa wametangaza kuwa matumizi ya bangi sio kosa la jinai.
No comments:
Post a Comment