Mchungaji na Mwalimu Christopher Mwakasege
jana Jumanne Oktoba 16, 2018 aliongoza maombi ya ibada ya kuaga mwili
wa mwanaye wa pekee wa kiume, Joshua Mwakasege. Ibada
iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Mbezi Beach
na kuhudhuriwa na mamia ya watu, akiwemo Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa.
Akiongoza maombi hayo, Mwakasege alisema; “Kabla ya kifo, niliwasiliana na Joshua, nilimuahidi kuwa tungezungumza tena jioni baada ya kumaliza semina. Nilipomaliza
semina nilimpigia simu lakini iliita bila kupokelewa. Baadaye mlinzi wa
kazini kwao alipokea na akatueleza kuwa Joshua amekimbizwa hospitali,”
amesema Mwakasege.
Joshua alifariki siku ya Alhamisi, 11 Oktoba 2018 baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini kwake World Bank, Dar es Salaam ambapo aliwahishwa hospitali ya Aga Khan na kufariki baadae usiku huo.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Joshua. Amen.
No comments:
Post a Comment