Thursday, March 15, 2018

SHONZA: WIMBO ULIOFUNGIWA NCHINI HAURUHUSIWI KUTUMIKA KATIKA SHOW ZA NJE YA NCHI

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza amesema sheria hairuhusu wimbo uliofungiwa nchini kutumika katika show nje ya nchi.

Naibu Waziri amesema hayo jana kupitia kipindi cha XXL cha Clouds ambacho kuliwakutanisha wasanii, Wizara na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

“Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kuufanyia show nje ya nchi. Endapo atafanya hivyo atakuwa anakiuka kanuni na sheria za nchi.” amesema Juliana Shonza.

Februari 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka BASATA na kuamuru nyimbo hizo kutopigwa katika vyombo vya habari.

No comments: