Thursday, March 15, 2018

WANAFUNZI WALIOTANGAZA NONDO KATEKWA WAHOJIWA POLISI; WAMEONGEA BAADA YA MAHOJIANO (VIDEO)

Hellen Sisya, Msemaji wa TSNP.
Jana 14 Machi 2018 viongozi wanne wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) wakiongozwa na Msemaji wa Mtandao huo Helen Sisya, wameitikia wito baada ya kutakiwa kufika kwa Mpelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuhusu suala la kupotea kwa Mwenyekiti wao Abdul Nondo.

Viongozi hao walifika kwa DCI na kufanya mahojiano wakiwa kama mashahidi kwa takribani zaidi ya saa 8 ambapo baada ya kutoka msemaji wao ameeleza kuwa wametoa ushirikiano huo kwa kuamini kuwa ni suala la kisheria.


No comments: