Serikali kupitia Wizara ya Nchi – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesimamisha utoaji huduma katika hospitali
zote za Marie Stopes Tanzania (MST).
Akizungumzia sababu za kusimamisha huduma hizo, Naibu Waziri wa
Tamisemi anayeshughulikia masuala ya afya, Josephat Kandege alisema kuwa
hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hospitali hiyo kukiuka miongozo.
Hata hivyo, Kandege alisema kuwa Mganga Mkuu wa Serikali ndiye
anaweza kutoa ufafanuzi zaidi wa kitaalam wa sababu za kufungiwa kwa
hospitali hizo.
“Mhusika ambaye atakuwa kwenye nafasi nzuri kuweza kulizungumzia
suala hili ni mganga Mkuu wa Serikali ili tuwe na taarifa sahihi ya
kuutarifu umma,” Kandege anakaririwa na Mwananchi.
Awali, msemaji wa MST, Dotto Mnyadi alisema kuwa hospitali hizo
zimesimamishwa kutokana na ukaguzi uliokuwa unaendelea kufanywa na
Serikali.
No comments:
Post a Comment