Wanafunzi 19 wamekufa na wengine makumi wamejeruhiwa baada ya
mwanafunzi mwenzao kuwafyatulia risasi katika chuo cha eneo la Crimea
nchini Urusi.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 18, anadaiwa kupita katika
vyumba kadhaa vya bweni la wanafunzi pamoja na mgahawa wa chuo hicho
akifyatua risasi hovyo.
Mshambuliaji huyo ambaye ametajwa kwa jina la Vladislav Roslyakov,
alijiua baada ya kufanya mauaji hayo, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa
na kamati maalum ya vyombo vya ulinzi vya Urusi.
Vyombo vya ulinzi na usalama vimeeleza kuwa mbali na shambulizi hilo
pia milio ya milipuko kadhaa ilisikika katika eneo hilo. Wapelelezi wa
tukio hilo wameeleza kuwa walibaini kuwepo kwa kilipuzi kimoja kwenye
mfuko wa mshambuliaji huyo.
Taarifa za awali zililitaja tukio hilo kama shambulizi la kigaidi,
lakini wapelelezi wa Urusi walieleza kuwa halikuwa na uhusiano na
ugaidi.
No comments:
Post a Comment