Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa,
Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
zimekutana kujadili suala la ufungaji kamera maalumu za kudhibiti na
kuzuia uhalifu.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa
ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera
hizo katika miji yote mikuu nchini.
Amesema kuwa lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali
kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani na
uporaji wa fedha katika taasisi za fedha.
“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari
wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi
zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu,”amesema Mhandisi Masauni.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za
Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid
Haroub amesema kuwa tayari washafunga kamera hizo ambazo zilizinduliwa
Oktoba 3, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment