Wednesday, May 2, 2018

MANARA ATOA UJUMBE TATA KWA WANA SIMBA

Image result for picha ya haji manara
Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amezua utata kwa wadau na mashabiki wa timu hiyo kufuatia ujumbe wenye mafumbo aliouandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mbali na kuandika kwa ujumbe huo, Manara vilevile amejiondoa kwenye makundi mengi yaliyo katika mtandao wa WhatsApp huku sababu zikiwa hazijulikani.

Taarifa za chini ya kapeti ambazo si rasmi zinaeleza yawezekana kukawa kuna masuala hayajakaa sawa baina yake na uongozi wa juu mpaka kuelekea kujitoa kwenye makundi hayo na kuandika ujumbe huo wenye utata.

"Nia yangu ni njema sana ila mimi pia nina nyongo, sihitaji heshima ila walau nipewe utu ninaostahili, nimefanya kwa kadri nilivyojaaliwa na Mungu ila lazima tusonge mbele kwa maslahi mapana ya klabu" ameandika Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ujumbe umekuwa ni mgumu kutafsirika na mpaka sasa umewaweka wadau midomo wazi kwa kushindwa kuelewa Manara anamaanisha nini.

Jitihahada za kumtafuta Manara ili aweze kulitolea ufafanuzi kauli hiyo zimegonga mwamba kutokana na simu yake kutokuwa hewani.

No comments: