Thursday, April 5, 2018

ROMA AJISAJILI RASMI BASATA (Angalia VIDEO)

Leo Aprili 05,2018 msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki amekutana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa mara nyingine tena ambapo safari hii amejisajili na kukabidhiwa rasmi cheti cha kutambulika na  (BASATA) kama msanii na hii ni baada ya kupewa sharti na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kusajili kwanza BASATA  ili aondolewe adhabu yake ya kufungiwa miezi sita.




Tarehe 1 Machi mwaka huu msanii Roma Mkatoliki alifungiwa kazi zake za sanaa na BASATA kwa miezi sita kutokana na wimbo wake wa “Kibamia” kutofuata maadili ya Kitanzania lakini Machi 29, 2018 Roma Mkatoliki alitangaza rasmi kuufuta wimbo huo baada ya kupata msamaha wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

No comments: