Mkurugenzi Mtendaji na Muanzilishi wa kituo cha Radio EFM na TVE, Francis Ceasar maarufu kama DJ Majizzo ametoa pongezi kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa kuingia rasmi kwenye Media Industry hapa Tanzania.
Majizzo amesema kuwa vituo vyake vya EFM na TVE vimejitahidi kuifikisha tasnia ya habari sehemu fulani hivyo anaamini kuwa ujio wa Wasafi TV na Radio vitaifikisha mbali tasnia ya habari.
"Ni mpango mzuri uliochukua na mimi binafsi nakupongeza juu ya kuchagua sekta ya vyombo vya habari, kama vijana ni wajibu wetu kuwahamasisha vijana wengine kufanya kazi kwa bidii ili kujenga taifa letu leo na kizazi cha baadae. Sisi kama “E” tumefanya kidogo na tunaamini kuwa Wasafi (TV na Radio) zitafanya mengi zaidi. Karibu tujenge Tanzania. Karibu kwenye tasnia ya habari @diamondplatnumz," ameandika Majizzo kwenye taarifa yake aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram.
Kituo cha Wasafi TV kinachomilikiwa na Diamond Platnumz kimeanza kurusha matangazo yake Jumatatu ya Aprili 02, 2018 na tayari wasanii na wadau wa muziki wameanza kutoa pongezi kwa kile wanachodai kuwa kituo hicho kimekuja kubadili mfumo dume wa upendeleo wa upigwaji wa ngoma za wasanii wa muziki.

No comments:
Post a Comment