Wednesday, April 25, 2018

HAKI ZA BINADAMU WATAJA KUPOTEA KWA AZORY


DAR ES SALAAM.  Mzimu wa kutoweka kwa mwandishi wa Mwananchi, Azory Gwanda umeibuka tena kwenye Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2017, iliyowasilishwa leo jijini Dar es Salaam.

Tangu Azory alipotoweka Novemba 21, mwaka jana bado hakuna taarifa za kupatikana kwake.

Akiwasilisha ripoti hiyo, Mtafiti wa Haki za Binadamu, Fundikira Wazambi amesema kutoweka kwa mwandishi huyo ambayo bado hajulikani alipo kumeleta taharuki miongoni mwa wanahabari.

Amesema matukio kadhaa ya vitisho na unyanyasaji wa wanahabari yaliripotiwa mwaka jana ikiwamo uvamizi wa ofisi za Clouds Media uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, vitisho na ukamataji wa wanahabari 10 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya mkoani Arusha.

"Magazeti manne yalifungiwa na kulipishwa faini, kwa sababu tofauti," amesema.

Amesema haki ya kupata taarifa ilihatarishwa kupitia kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kutoa maoni.

No comments: