Thursday, April 5, 2018

ALI KIBA AIBUKIA WASAFI



Msanii wa Bongo Flava, Alikiba. PICHA | FILE
DAR ES SALAAM.  Kama ulikuwa unadhani nyimbo za Ali Kiba hazitachezwa katika televisheni ya Wasafi inayomilikiwa na kampuni ya WCB utakuwa umekosea sana.

Jana televisheni hiyo ambayo Afisa Mtendaji wake Mkuu, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz ilicheza nyimbo za Ali Kiba.

Televisheni hiyo inayoonekana katika kingámuzi cha Azam ilianza majaribio ya kurusha matangazo yake Aprili 2, 2018.

Kuchezwa kwa nyimbo za Ali Kiba ni wazi kutakuwa kumewapa jibu wapenzi wa muziki wa Bongo fleva nchini kutokana na kwamba wawili hao mara kwa mara kuelezwa kuwa na ushindani.

Mambo ni tofauti, nyimbo mbalimbali za Ali Kiba kwa siku nzima ya leo zimekuwa zikipigwa katika televisheni hiyo.

Mwandishi nguli wa habariza michezo wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) inayochapsha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, Edo Kumwembe kupitia ukurasa wake wa Instagram juzi aliweka ujumbe uliozua mjadala.

Ujumbe huo ulioambatana na picha ya logo ya Wasafi TV unasomeka, "Naam watazamaji wetu wa Wasafi TV katika countdown yetu leo wimbo ulioshika namba moja ni Seduce me kutoka kwa Ali Kiba."

Baadhi ya wachangiaji waliungana na Edo na wengine walimpinga lakini jana Edo tena kupitia ukurasa wake huo ameweka ujumbe ukiambatana na picha aliyoipiga ikionyesha wimbo wa Ali Kiba ukipigwa kwenye Wasafi TV.

Edo amesema, "Jana watu walitoka povu humu... anyway Diamond Platnumz ni professional musician na mfanyabiashara anayejua anachokifanya."

No comments: