Wednesday, March 14, 2018

SIMBA YATANGAZA KIKOSI CHAKE


Klabu ya soka ya Simba imetangaza kikosi kitakachoondoka leo kuelekea Misri kwaajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.

Mkuu wa idara ya habari ya klabu hiyo, Haji Manara amewataja viongozi 7 ambao wataongozana na timu kuwa ni Kocha mkuu Pierre Lichantre, kocha msaidizi Masoud Juma kocha wa viungo Muharam Mohammed na Mohammed Aymen.

Wengine ni daktari wa timu Dr. Yassin Gembe, meneja wa timu Richard Robert na Yassin Mtambo ambaye ni mtunza vifaa. Mchezo huo utapigwa jumamosi Machi 17 huko jijini Port Said Misri.

Wachezaji ni James Kotei, Yusufu Mlipili, Emanuel Okwi, Laudit Mavugo, Shomari Kapombe, Said Hamisi, Mohamed Hussein, Asante Kwasi na Erasto Nyoni. Wengine ni Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, John Bocco, Paul Bukaba, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya, Nicholas Gyan, Said Mohamed 'Nduda', Aishi Manula, Juuko Murushid na Juma Luizio.

Msafara huo unatarajia kuondoka leo saa 10:00 jioni huku mkuu wa msafara akiwa ni Kaimu Rais wa Simba Dr. Salim Abdallah. Simba na Al Masry zilitoka sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

No comments: