Wednesday, March 21, 2018

KAULI YA SERIKALI KUHUSU AFISA UBALOZI ALIYEVAMIWA NA KUIBIWA DSM

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba Afisa Ubalozi wa Ubalozi wa Syria nchini H. Alfaori amevamiwa na kuibiwa mchana wa leo March 20, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Serikali Dr Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kuwa Afisa huyo H. Alfaori alishambuliwa na watu watatu wenye silaha kwenye viunga vya Oysterbay majira ya saa nane mchana na kuporwa fedha taslimu Euro 93,000 sawa na Shilingi Milioni 251 za Kitanzania pamoja na gari ya Ubalozi aina ya Hyundai.

Serikali imesema kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za shambulio hilo na kwamba kwa sasa Afisa huyo amelazwa Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu.

No comments: