Wednesday, March 21, 2018

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI BODI YA NHC

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu asubuhi ya leo Machi 21, 2018 ni kwamba Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Blandina Nyoni kuanzia leo.

Pia Rais Magufuli ameivunja Bodi ya shirika hilo la NHC.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uteuzi wa Mwenyekiti mpya na Bodi nyingine utafanyika baadaye.

Wakati huo huo, Rais Magufuli pia leo atawaapisha Mabalozi Wateule wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli atamuapisha IGP-Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.

Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi Wateule hao itafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi.

No comments: