Wednesday, March 21, 2018

BREAKING NEWS: ABDUL NONDO AFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA

Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi TSNP, Abdul Nondo amefikishwa leo katika Mahakama ya Wilaya  Iringa kusomewa mashtaka yanayomkabili. 

Taarifa zilizotolewa na Wakili wake, Jebra Kambole leo Jumatano Machi 21, 2018 zinaeleza kuwa asubuhi ya leo Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Iringa baada ya kusafirishwa siku wa kuamkia leo kupelekwa huko mkoani Iringa.

Nondo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 na siku iliyofuata akaonekana mjini Mafinga, wilayani Mufindi, Iringa ambako alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kurejeshwa Dar es Salaam.

No comments: